Exness Review 2026: Uchambuzi wa Exness Broker Tanzania

July 16, 2026
Broker Reviews

Exness ni miongoni mwa broker wakubwa na maarufu zaidi duniani, na kwa sasa amekuwa chaguo la wengi hapa Tanzania. Kwenye review hii tutachambua kwa kina kila kitu unachotakiwa kujua kuhusu Exness broker, kuanzia gharama za trade, aina za account, platform zake, mpaka usalama wa pesa zako, ili uweze kufanya maamuzi sahihi kabla hujajiunga.

Exness ni nani?

Exness ni broker mwenye zaidi ya wateja 800,000 duniani kote, na mzunguko wa trade unaozidi dola trilioni 3 kwa mwezi. Alianzishwa mwaka 2008, na kwa miaka yote hii amejijengea jina kubwa. Kupitia Exness unaweza ku trade forex pamoja na CFDs za hisa, indices, crypto na commodities kama dhahabu na mafuta, kwa bei za ushindani.

Kitu kizuri ni kwamba ana account za kila aina, iwe wewe ni mwanzo kabisa au tayari ni trader mzoefu. Ila tuseme ukweli, kama wewe ni beginner kabisa unayehitaji kufundishwa hatua kwa hatua, Exness hana rasilimali nyingi za elimu kama walivyo baadhi ya broker wengine.

Bei, Spread na Gharama za Exness

Hili ndilo swali la kwanza kwa kila trader, gharama zikoje? Ukweli ni kwamba Exness ana spread nzuri za ushindani, ila gharama halisi utakayolipa inategemea aina ya account uliyonayo na unatrade instrument gani.

Kwenye Standard na Standard Cent account, spread zinaanzia pip 0.3, na huna commission yoyote bila kujali unatrade volume kiasi gani. Tofauti kubwa kati ya hizi mbili ni kwamba Standard Cent imetengenezwa mahsusi kwa wanaoanza, ikitumia micro lots ili usihatarishe pesa nyingi.

Kwa upande wa account za kitaalamu (professional), zipo tatu:

  • Raw Spread Account — spread kuanzia pip 0.0, na commission hadi dola 3.50 kila upande kwa lot moja.
  • Zero Account — spread kuanzia pip 0.0, ila commission ndogo zaidi, kuanzia dola 0.2 kila upande.
  • Pro Account — hii ndiyo nzuri zaidi kwa wengi: spread kuanzia pip 0.1 na commission 0%.

Swap na gharama za usiku

Baadhi ya instrument kama crypto na hisa ni swap-free moja kwa moja. Nyingine zina gharama ya rollover ukishikilia position mpaka usiku. Ila habari njema kwa Waislamu na wale wanaotaka kutrade bila riba, Exness ana Swap-Free account ambazo hazina gharama za ziada za riba, kulingana na taratibu za Kiislamu.

Gharama zingine

Jambo linalompa Exness pointi kubwa ni kwamba hatozi gharama yoyote pale unapoweka au kutoa pesa. Pia hana inactivity fee. Ila kumbuka: account za MT4 zitazimwa ukikaa siku 180 bila kuzitumia, na za MT5 zitaondolewa baada ya siku 21 tu za kutozitumia.

Kuweka na Kutoa Pesa (Deposit & Withdrawal)

Hapa ndipo Exness anang'ara kwa traders wa Tanzania. Kuweka na kutoa pesa ni bure kabisa, hakuna makato. Na njia za malipo ni nyingi: bank card, crypto wallets, pamoja na eWallets kama Neteller, Skrill na Perfect Money.

Kiasi cha chini cha kuweka kinaanzia dola 10 tu ukitumia bank card. Baada ya ku verify taarifa zako za utambulisho, utapelekwa kwenye eneo la exness login ambapo ndipo unasimamia account zako zote na settings za platform. Kwa upande wa kutoa, kiwango cha chini kinaanzia dola 1 kupitia baadhi ya njia.

kabla hujajiunga, hakikisha unaangalia kama njia unayopendelea (kama M-Pesa, Tigo Pesa au Airtel Money kupitia mawakala) inapatikana kwa eneo lako, kwa sababu njia za deposit na withdrawal zinaweza kutofautiana kutegemea nchi uliyopo.

Platform za Kutradia

Exness ana exness terminal yake mwenyewe, ambayo ni web platform iliyotengenezwa na wataalamu wake wa ndani kwa kutumia teknolojia ya HTML5. Terminal hii imeunganishwa na TradingView, kwa hiyo unapata tools nzuri za uchambuzi na aina mbalimbali za order. Ni ya haraka, ya kuaminika, na rahisi kutumia hata kwa simu.

Zaidi ya hapo, Exness pia anatoa MetaTrader 4 (MT4) na MetaTrader 5 (MT5). Kati ya hizi, MT4 ndiyo inayopendwa zaidi na matrader wa Exness kutokana na spread nzuri za forex.

Pia kuna Exness Trade App, application ya simu yenye zaidi ya instrument 200 za forex, crypto, indices, hisa na energies. Kwa ujumla, ukichagua Exness huna wasiwasi wa platform, kila mtu atapata inayomtosha kulingana na style yake ya kutrade.

Aina za Account za Exness

Exness ana aina mbili za Standard account na tatu za professional:

Standard:

  • Standard Account
  • Standard Cent Account (nzuri kwa wanaoanza)

Professional:

  • Raw Spread Account
  • Zero Account
  • Pro Account

Kama wewe ni mwanzo, anza na Standard au Standard Cent. Ukishakuwa na uzoefu na unataka spread ndogo zaidi, ndipo uhamie kwenye professional accounts.

Elimu na Utafiti (Research & Education)

Kwenye upande wa elimu, Exness ana academy yake kwenye insights.exness.com yenye makala zinazoelezea dhana za msingi za trading, saikolojia ya soko, strategy na habari. Ila kwa uaminifu, baadhi ya sehemu hizi hazijaupdatiwa kwa miezi kadhaa. Kwa hiyo kama wewe ni beginner, huenda ukahitaji kutafuta elimu ya ziada sehemu nyingine.

Where Exness anafanya vizuri zaidi ni kwenye research na tools za uchambuzi. Anakupa trading signals na uchambuzi wa kiufundi (technical) na wa kimsingi (fundamental) kupitia Trading Central. Pia kuna market news kutoka FXStreet. Vyote hivi vinapatikana kwenye client area au moja kwa moja kwenye Exness Trade App.

Usalama na Udhibiti (Regulation)

Hili ni muhimu sana, hasa ukizingatia kwamba Tanzania kwa sasa haina mamlaka rasmi inayodhibiti broker wa forex wa ndani. Kwa sababu hiyo, ni lazima uchague broker aliyedhibitiwa na mamlaka zenye majina makubwa nje ya nchi.

Exness anasimamiwa na mamlaka kadhaa zinazoheshimika duniani:

  • CySEC ya Cyprus
  • FCA ya Uingereza
  • FSCA ya Afrika Kusini
  • FSA ya Seychelles

Hii inaonyesha kwamba pesa zako zipo kwenye mikono salama. Ila Exness bado hajadhibitiwa na mamlaka yoyote ya ndani hapa Tanzania, jambo ambalo linaweza kuwakwaza baadhi ya watu.

Huduma kwa Wateja (Customer Support)

Exness anafanya vizuri hapa pia. Anatoa msaada saa 24 kwa siku, siku 5 kwa wiki, kwa lugha 14. Kwa lugha ya Kiingereza, msaada unapatikana saa 24/7.

Njia za kupata msaada:

  • Live chat kupitia website. kawaida unapata majibu ndani ya siku hiyo hiyo.
  • Simu, kwa mambo ya haraka: +35725245730
  • Email: support@exness.com

Hitimisho: Je, Exness Anafaa?

Mambo mazuri ya Exness ni spread ndogo za forex, leverage kubwa kwenye baadhi ya instrument, na huduma nzuri kwa wateja. Ni miongoni mwa broker wakubwa zaidi duniani kwa volume na idadi ya wateja, na anazidi kupata umaarufu hapa Afrika Mashariki, ikiwemo Tanzania.

Kwa upande mwingine, hana leseni ya ndani ya Tanzania, na orodha yake ya instruments si pana kama baadhi ya broker wengine. Kama unatafuta vitu kama ETFs au hisa za kampuni za ndani, hutavipata kwa Exness.

Kwa kifupi: tunapendekeza Exness broker kwa matrader wa kati (intermediate) wanaotafuta broker wa kuaminika, mwenye uwepo mkubwa duniani, leverage kubwa, na gharama nzuri za kutrade. Kama wewe ni mwanzo kabisa, unaweza kuanza naye pia, ila jipange kutafuta elimu ya ziada sehemu nyingine.

Onyo la Hatari: Biashara ya forex na CFDs ina hatari kubwa. Unaweza kupoteza mtaji wako wote. Usitrade kwa pesa ambayo huwezi kumudu kuipoteza, na daima fanya utafiti wako mwenyewe kabla ya kuwekeza.

Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara (FAQ)

Je, unaweza kupata faida kwa kutrade na Exness?
Ndiyo, kwa strategy nzuri unaweza kuwa miongoni mwa maelfu ya matrader wanaopata faida na Exness. Ila kumbuka trading ina hatari.

Je, Exness ni halali Tanzania?
Ndiyo, kutrade na Exness ni halali. Anasimamiwa na mamlaka kubwa za kimataifa, ingawa hana leseni ya ndani ya Tanzania kwa sasa.

Je, Exness ni salama?
Ndiyo, Exness ana kiwango cha juu cha usalama kwa sababu anadhibitiwa na mamlaka kadhaa za daraja la juu duniani kama CySEC, FCA, FSCA na FSA.

Je, Exness ni broker wa kuaminika?
Ndiyo, Exness ni broker halali na wa kuaminika, mwenye udhibiti kutoka mamlaka mbalimbali duniani kote.

Sam R.

Sam R. ni mchambuzi wa fedha mwenye uzoefu wa miaka 5+ katika masoko ya fedha ya kimataifa, akijikita hasa katika masoko ya Afrika Mashariki. Ana utaalamu wa uchambuzi wa kiufundi (technical analysis) na uchambuzi wa msingi (fundamental analysis) katika Forex, Hisa, Dhahabu, na Indices.

Kabla ya kuanzisha BingwaFX, Sam alifanya kazi kama mshauri wa uwekezaji kwa wateja wa biashara wa Tanzania na Kenya, akisaidia kampuni na watu binafsi kuelewa hatari za masoko ya fedha na jinsi ya kusimamia rasilimali zao vizuri. Uzoefu huo wa vitendo ndio msingi wa kila makala anayoandika, kila uchambuzi anaotoa, na kila onyo la hatari analolisema.

Lengo lake kuu ni moja: kufanya biashara ya fedha ieleweke kwa Watanzania kwa lugha yao wenyewe. Mengi ya maarifa ya masoko ya fedha yanaandikwa kwa Kiingereza, na hii inawakosesha fursa watu wengi wa Afrika Mashariki ambao wana akili na mtaji wa kuwekeza lakini hawana mwongozo wazi. BingwaFX ni jibu lake kwa tatizo hilo.

Related Posts

Jiunge Nasi

Thank you! Your submission has been received!

Oops! Something went wrong while submitting the form